Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miraji ataja mastraika wake hatari

Miraji ataja mastraika wake hatari

Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BEKI wa Ndanda FC, Miraji Adam ametaja washambuliaji sita ambao amebainisha kuwa tangu ameanza kucheza soka ameona hawana masihara wanapokuwa karibu na goli. Miraji ambaye aliwahi kuchezea Simba, Coastal Union, Singida United alimtaja Roberto Lewandoski wa Bayen Munich, Luis Suarez  wa FC Barcelona, Edson Cavan anayeichezea  PSG, Amis Tambwe  wa Fanja na Meddie Kagere wa Simba.. Miraji alisema tangu ameanza kufuatilia na kucheza soka ameshuhudia nyota hao kuwa ndio wapambanaji zaidi na hawawezi kukuacha salama ukiwaacha wakafika eneo la hatari. "Hao ndio washambuliaji ambao nimepata kuwaona na kushuhudia upambanaji wao, hawana masihara kabisa wanapokuwa karibu na goli ni lazima wakulize umakini kwao unatakiwa kuwa ndani ya dakika zote za mchezo ukiwapa upenyo ata kidogo umekwisha," alisema. "Nawakubali sana na ndio maana nimewataja na miongoni mwao kwa nyota hao wawili Tambwe na Kagere nimekutana nao na kupambana nao hivyo ugumu wao na ubora wao nautambua sio kwa kuwaona ni kwa kucheza nao uwanja mmoja," alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz