Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miquissone: Nitapambania klabu yangu, heshima na mashabiki

SIMBA 8 1?fit=1080%2C722&ssl=1 Miquissone: Nitapambania klabu yangu, heshima na mashabiki

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MASAA machache yamesalia wekundu wa Msimbazi Simba, kutimua nyasi za Uwanja wa Benjamin Mkapa huku nyota mahiri wa kikosi hicho Luis Miquissone akitamba kupambana vilivyo kupata matokeo.

Simba ni mwenyeji wa Kaizer Chiefs mchezo wa robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika mchezo utakaopigwa saa 10:00 jioni huku Wekundu hao wakitakiwa kupata ushindi wa mabao 5-0 baada ya awali kupoteza kwa mabao 4-0.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Miquissone ameandika kuwa, atapambana kwa ajili ya klabu yake iweze kupata matokeo katika mchezo huu.

"I will fight for my club, my legacy history and for my people, it's matchday,"akimaanisha nitapambana kwa ajili ya klabu yangu, heshima, historia na mashabiki kwenye mechi ya leo

Naye Mtendaji Mkuu wa kikosi hicho Barbara Gonzalez amesema, watapambana kupata mabao 5-0 ili waweze kusonga mbele akimtanguliza Mungu.

"Ee mwenyezi Mungu tunakuomba utufanyie wepesi leo katika mchezo wetu, uwape wepesi wachezaji wetu wote wapambane tupate ushindi wa magoli matano na kuendelea In shaa Allah," amesema na kuongeza kuwa tunakuomba Mwenyezi Mungu utujalie tufuzu hakuna kisichowezekana.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz