Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Minziro, Choki waibukia Geita Gold

TIMU YA GEITA GOLD Minziro, Choki waibukia Geita Gold

Mon, 31 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Saddam SadickMWANZA. WAKATI dirisha la usajili likifungwa usiku wa leo, huko Geita Gold wamejihakikishia kupata huduma ya Makocha Fred Felix ‘Minziro’ na Choki Abeid waliowanyakua ili kuingoza timu yao kwa msimu ujao wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Minziro aliyeshuka na Mbao FC kupitia Play Off kwa tofauti ya bao la ugenini dhidi ya Ihefu, aliweka rekodi ya kushinda mechi nane kati ya michezo 10 aliyosimamia akiwa na timu hiyo kwa kutoa sare moja na kupoteza mechi moja na kujishindia Tuzo ya Kocha Bora wa Julai.

Geita Gold kwa takribani misimu minne, imekuwa ikihaha kupanda Ligi Kuu, lakini imekuwa ikiishia hatua za Play Off, hata msimu uliopita ilijikuta ikitolewa na Mbeya City kwa mabao 2-1.

Mwanaspoti, imepenyezewa kuwa Minziro ameitosa Mbao na sasa atakuwa Kocha Mkuu, huku Abeid ambaye aliyekuwa Gipco pia ya Geita iliyomaliza nafasi ya nne katika FDL atakuwa msaidizi wake.

Wawili hao wamekuwa na historia nzuri katika soka la hapa nchini na Minziro atakumbukwa kwa kazi nzuri ya kuzipandisha timu kadhaa, ikiwamo KMC na Singida United.

Akizungumza na gazeti hili baada ya kutia saini ya mwaka mmoja, Kocha Abeid alisema kwa sasa wanajiandaa kuanza mazoezi ya pamoja na malengo yao ni kuipandisha timu Ligi Kuu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz