Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Milambo ajivunia ubora wa Serengeti Boys

49002 Pic+milambo

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Milambo amesema michezo ya kirafiki waliocheza na Ngorongoro Hereos imewapa ukomavu vijana wake.

Milambo alisema vijana wake wanaendelea kuimarika kupitia aina ya mazoezi ambayo wamepewa na Ngorongoro Heroes kwenye michezo mitatu ambayo wamecheza ya kirafiki.

Kocha huyo alisema kupitia michezo hiyo atafanyia kazi mapungufu ambayo ameyaona ili waweze kufanya vizuri katika mashindano ya Afcon kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17.

"Huu wa leo tumefungwa mabao sita kwa mbili ni mchezo wetu wa tatu, miwili iliyopita tulishinda. Naamini uzoefu wa Ngorongoro utakuwa umewajenga vijana wangu.

"Kuna mapungufu ambayo kama mwalimu nimeyaona na nitayafanyia kazi, lengo letu ni kutwaa ubingwa wa mashindano hayo, " alisema Milambo.

Milambo alisema matarajio ya kuwa na michezo mingine ya kimataifa ya kirafiki kabla ya kuanza kwa mashindao ya Afcon kwa vijana nchini Aprili 14-28, 2019.



Chanzo: mwananchi.co.tz