Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikwaju ya penati imeiua Zanzibar vs Kenya fainali leo

Sun, 17 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes Jumapili ya December 17 2017 ilikuwa mjini Machakos Kenya kucheza mchezo wake wa fainali ya michuano ya CECAF Senior Challenge Cup dhidi ya timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars.

Zanzibar ndio wawakilishi pekee wa Tanzania waliyokuwa wamefanikiwa kufika hatua ya mbali baada ya wenzao wa Tanzania bara Kilimanjaro Stars kutolewa katika hatua ya makundi, kwa bahati mbaya leo licha ya Zanzibar kufanya vizuri katika game zake zote zilizopita leo bahati haikuwa yao na wamepoteza.

Timu ya Zanzibar Heroes imepoteza mchezo kwa mikwaju ya penati 3-2, hiyo ni baada ya dakika  120 kumalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2, magoli ya Zanzibar yakifungwa na Hamisi Musa dakika ya 87 na 99 wakati magoli ya Kenya yakifungwa na Ochieng Ovella dakika ya 5 na Choka Masoud dakika ya 97.

Pamoja na Zanzibar Heroes kupoteza mchezo huo kwa mikwaju ya penati wizara ya michezo Zanzibar imewaandaliwa mapokezi maalum kesho saa 3:00 watakapowasili Zanzibar wakitokea Kenya.

Mstaafu Kikwete na Zitto Kabwe baada ya Zanzibar kuingia fainali

Chanzo: millardayo.com