Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Michuano ya Samia Cup kuanzishwa

Michuano Ya Samia Cup Kuanzishwa.png Michuano ya Samia Cup kuanzishwa

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema katika kuenzi na kuthamini mchango mkubwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Michezo, Wizara imeshavielekeza vyama na mashirikisho ya michezo nchini viangalie namna kuwa na kombe maalum la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika michezo wanayoisimamia.

Mhe. Mwinjuma ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma jana Agosti 27 2024 wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum, Mhe. Aziza Sleyum Ally aliyetaka kujua namna Serikali ilivyojipanga kuanzisha kombe maalum la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa anajitoa sana kwenye Sekta ya michezo nchini.

Mhe. Mwinjuma amesema lengo la kuwaelekeza mashirikisho ya michezo kuwa na kombe maalumu la Dkt.Samia ni kuwa na mashindano makubwa ya kitaifa yatakayohusisha michezo mbalimbali yatakayofahamika kama Samia Taifa Cup kuanzia ngazi ya chini na tayari wizara imegawa vifaa katika mikoa yoteTanzania Bara na Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live