Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Michuano ya CECAFA yapeleka kilio Azam FC

445 MBARAKA 13 TZW

Wed, 20 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Mbaraka Yusuph kulia kwenye picha.

Klabu ya Azam FC leo imetangaza rasmi kuwa itamkosa kwa muda mshambuliaji wake, Mbaraka Yusuph ambaye anapelekwa nchini Afrika Kusini kwaajili ya matibabu ya majeraha aliyoyapata akiwa na timu ya taifa katika michuano ya CECAFA iliyomalizika wikiendi iliyopita.

Taarifa hizo zimethibitishwa na Msemaji Mkuu wa klabu hiyo, Jaffery Iddy Maganga ambapo amesema Mchezaji huyo baada ya kurejea nchini akitokea Kenya, daktari wa timu alimfuatilia kwa karibu afya yake na imeonekana kuwa hatoweza kuitumikia klabu yake mpaka pale atakapofanyiwa vipimo vikubwa nchini Afrika kusini.

Hii inakuwa mara ya pili kwa mshambuliaji huyo kuumia akiwa na timu ya Taifa ambapo mara ya kwanza aliumia katika michuano ya COSAFA iliyofanyika nchini Afrika Kusini mwezi Juni mwaka huu.

“Mtakumbuka Mbaraka Yusuph alikuwa na timu ya Taifa nchini Kenya katika michuano ya Challenge na kwa bahati mbaya akaumia na vipimo vimeonyesha ameumia sehemu ya goti na hawezi kucheza, tayari uongozi wa juu umetoa ruhusa kwa Mbaraka kupelekwa Afrika kusini kwaajili ya vipimo na matibabu.” amesema Maganga.

Chanzo: bongo5.com