Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Michezo kuhamamsisha utunzaji wa mazingira

Kjqbzwrivk6wre6062fc5a6a923.jpeg Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango anatarajia kuwaongoza wanariadha zaidi ya 2000 kwenye mbio za Mazingira marathoni zitakazofanyika Novemba 14 kwa mara ya kwanza nchini.

Wanariadha wa ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kukimbia kwenye mbio hizo zitakazoanzia na kumalizikia kwenye viwanja vya green ground maarafu kama uwanja wa farasi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa mbio hizo, Dr. Amon Mkoga amesema kuwa mbio hizo zinalenga kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhifadhi mazingira nchini.

Amesema wanariadha watachuana katika mbio za nusu marathoni (kilomita 21), kilomita 10 na kilomita tano ambayo makamu wa rais pia atakimbia mbio hizo.

"Maandalizi yameanza kwa wakimbiaji kujiandikisha kwa njia ya mtandao, mbio hii mbali na kuhamasisha utunzaji wa mazingira ambao utakwenda sanjari na upandaji miti, pia utasaidia vifaa vya uzazi kwa wa kina mama.

"Katika utoaji vifaa, tunashirikiana na TASAF na vifaa hivi vitatolewa kwa kaya masikini kwenye maeneo mbalimbali nchini," amesema.

Mmoja wa wasanii kwenye mbio hiyo, Haruna Kahena 'Inspector Haroun' ambaye ni miongoni mwa watakaokimbia mbio za kilomita 5 alisema anatamani mabingwa wote watoke nchini.

Amesema mbali na mbio hiyo kuwashindanisha wakimbiaji nyota nchini, lakini pia ni sehemu ya mazoezi.

Chanzo: eatv.tv