Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhini kuongoza timuya kuogelea Tanzania mashindano ya vijana Budapest

56295 Pic+buda

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Muogeleaji nyota nchini, Dennis Mhini ni miongoni mwa waogeleaji saba waliochaguliwa na chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania (TSA) kuunda timu ya Taifa itakayo wania taji la michuano ya Dunia iliyopangwa kufanyika nchini, Hungary.

Mhini ambaye kwa sasa anasoma na kuogelea katika shule ya St Felix ya Uingereza, ataungana na waogeleaji wenzake, Delvin Barick wa klabu ya Mwanza na muogeleaji wa kike, Kayla Temba  ambaye anatokea klabu ya DSC.

Waogeleaji wengine ni Laila Rashid kutoka klabu ya Taliss-IST, Christopher Fitzpatrick (Mwanza), Christian Shirima (DSC) na  Khaleed Ladha wa  Taliss-IST.

Gharama za usafiri, maradhi na mahitaji mengine kwa waogeleaji watatu, Mhini, Delvin na Kayla zitatolewa na Shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani (Fina) wakati waogeleaji wanne,  Laila, Fitzpatrick , Christian Shirima na   Khaleed  wanatakiwa kusafirishwa na TSA kwa kushirikiana na wadau.

Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro alisema kuwa Fina imewapa fursa ya kuwakilishwa na waogeleaji wengine kutokana na kuridhishwa na maendeleo ya mchezo wa kuogelea nchini.

Inviolata alisema kuwa ni vigumu kuamini hivyo kutokana na changamoto zinazoukabili mchezo, ikiwemo ukosefu wa bwawa la kuogelea la kisasa, lakini bado waogeleaji wa Tanzania wamefanikiwa kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa.

“Tunahitaji sapoti kutoka kwa wadau, kwani Fina ipotayari kuwasafirisha waogeleaji watatu na kocha wao tu. Hawa waliobaki ni kazi ya TSA na wadau, hata hivyo TSA haina fedha kutokana na kuingia madarakani miezi kadhaa iliyopita,” alisema Inviolata.

Mhini kuongoza timuya kuogelea Tanzania mashindano ya vijana Budapest

Wednesday May 8 2019

By Mwandishi wetu

Chanzo: mwananchi.co.tz