Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgosi: Najivunia mafanikio ya Samatta

44673 Pic+mgosi Mgosi: Najivunia mafanikio ya Samatta

Tue, 5 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema anajivunia mafanikio ya Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji ambaye amepiga hatua zaidi yake aliyekuwa mfano hai kwake kwenye soka.

Mgosi ambaye kwa sasa ni kocha wa kikosi B cha Simba, alisema alimfanya Samatta kuwa rafiki kipindi ambacho alitua kwenye timu hiyo na yeye akiwa mshambuliaji wa kutegemewa.

“Kilichonisukuma kuwa naye karibu ni baada ya kutambua kuwa anatamani kufuata nyayo zangu, siku na kinyongo zaidi ya kumshauri na kumjenga pale ambapo alikuwa akikutana na changamoto ya kutopata namba.

“Alikuwa msikivu sana Samatta na muda wake uliopofika ndani ya ndani ya kipindi kifupi akafanya makubwa ndipo ulipokuwa mwanzo wake wa soka la kimataifa kwa kusajiliwa na TP Mazembe.

“Alivyojiunga na TP Mazembe nilienda kule na kukaa naye chini tena kwa sababu alikuta kuna utawala wa Trésor Mputu, nilimweleza awe mvumilivu nadhani matunda yake ni ile tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani,” alisema Mgosi.

Mshambuliaji huyo na nahodha wa zamani wa Simba, alisema wachezaji wengine wa Kitanzania wanatakiwa kuwa na uchu wa mafanikio kwa kufika mbali zaidi ya wachezaji wanaowakubali.

Mgosi alisema unaweza kuanza taratibu kwa kujiwekea malengo ambayo nyuma yake yanatakiwa kuwa na jitihada ya kufika mbali kama ilivyokuwa kwa Samatta ambaye hadi leo nimekuwa na mawasiliano nayo.

Samatta ambaye alianzia soka lake African Lyon kabla ya kutua Simba, ni kinara wa mabao Ligi Kuu Ubelgiji ambayo ni maarufu kama Jupiler Pro akiwa na mabao 20 kabla ya mchezo wa jana ambapo alikuwa akiongoza Genk mbele ya Sporting Charleroi.



Chanzo: mwananchi.co.tz