Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgeveke: Si kazi rahisi, Mwadui itabaki VPL

Mgeveke Pic Data Mgeveke: Si kazi rahisi, Mwadui itabaki VPL

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

NAHODHA wa Mwadui FC, Joram Mgeveke amekiri kuumizwa na nafasi ya mkiani iliopo timu hiyo na kwamba wanaumiza kichwa namna ya kujinasua ili kumaliza msimu wakiwa salama na kushuka daraja.

Mwadui FC imecheza  mechi 24, imeshinda nne, sare nne na imefungwa 16, kwa matokeo hayo imejikusanyia alama 16 zinazowafanya wawe mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na ikiwa imefungwa mabao mengi zaidi (43) kuliko timu nyingine.

Mgeveke ameliambia Mwanaspoti leo Jumanne ya Machi 30, 2021 kwamba hawajakata tamaa licha ya kukaa mkiani, wanachokifanya nikuelekeza nguvu kupigania pointi za michezo iliopo mbele yao.

"Najua sio kazi nyepesi, lakini tutapambana, tutajitoa kuona mechi zilizosalia zinatusaidiaje kumaliza msimu huu tukiwa tunaiacha timu salama, kiukweli ligi ni ngumu ambayo haitakiwi kujibweteka kila tunapocheza mechi," amesema na ameongeza kuwa;

"Kilichotuangusha ni ugeni wa baadhi ya wachezaji kwenye kikosi chetu, hivyo walikuwa hawana uzoefu na ushindani wa ligi, ingawa kwasasa naona wameanza kukaa katika mstari ambao wangekuwa hivyo tangu mwanzo sidhani kama tungekuwa hapa," amesema.

Amesisitiza kwamba wanahamasishana wenyewe kwa wenyewe kulinda heshima ya kazi yao, hivyo wanaamini chini ya kocha Amri Said wataisaidia timu kubakia ligi kuu.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz