Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Method Mwanjali apewa mkono wa kwaheri Msimbazi

473 20986777 483494468674032 43192566245490688 N TZW

Thu, 21 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya soka ya Simba SC imethibitisha kuachana na beki wao kisiki ambaye pia alikuwa kepteni wa timu hiyo kutoka nchini Zimbabwe, Method Mwanjali.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Zakaria Hanspoppe amethibitisha taarifa hiyo kwa kusema kuwa mchezaji pekee aliyeachwa katika dirisha hili dogo la usajili ni Mwanjali.

“Mchezaji aliyeachwa Simba ni Mwanjali peke yake, hakuna mchezaji mwingine aliyeachwa au aliyeongezwa Simba,” amesema Hanspope.

Wakati huo huo Mwenyekiti huyo wa usajili ameongezas kuwa tayari wamewasilisha barua kwa Lipuli FC kwa ajili ya maombi ya kumsajili mchezaji Asante Kwasi ambaye usajili wake umezua utata na kuteka vichwa vya habari hivi karibuni.

Chanzo: bongo5.com