Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mengine mapya kutoka kwa Haji Manara

Manara122 Haji Manara

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku moja baada ya aliyekuwa Msemaji wa Simba Sport club, Haji Manara kuongea na vyombo vya habari, alipoeeleza sakata zima la yeye kuachia ngazi klabuni humo, ameibuka hii leo tena katika mitandao ya kijamii akiwashtumu watu wanaosuka njama ya kum-unfollow katika mitandao ya kijamii.

Manara amewataka watu hao kuondoka mara moja katika kurasa zake kwani anamini watu walimfuata katika kurasa zake ni wale wenye mapenzi na yeye na sio mamluki.

Ameongeza kusema kuwa wakiondoka wafuasi 10 watakuja wapya 1000, hivyo kwake hilo sio tatizo, amepiga tambo zaidi kwa kuwaambia hao aliowatuhumu kwa njama hiyo wajitahidi wajibu kwa hoja na waache vioja vya aina hiyo kwani kwake Mungu ndiye Alpha na Omega.

Manara ameitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2015 hadi 2021 akitimiza miaka sita ya utumishi kama afisa mawasiliano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live