Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meddie Kagere awaita Yanga

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nakuru. Kinara wa mabao katika michuano ya SportPesa Super Cup, Meddie Kagere amewataka vigogo wa Yanga kuzungumza naye kwa kuwa yuko tayari kujiunga na klabu hiyo kongwe nchini.

Mshambuliaji huyo nguli, alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuipa Gor Mahia ubingwa wa michuano ya SportPesa katika mchezo wa fainali ambao timu hiyo ilishinda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Afraha, mjini Nakuru.

Yanga inammezea mate nyota huyo aliyefunga mabao manne kwenye mechi tatu za Gor Mahia na kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo.

Kagere aliyefunga bao moja katika mchezo wa juzi walipoifunga Simba mabao 2-0, alisema baada ya kuipa Gor Mahia mafanikio, yuko tayari kuzungumza kuhusu mustakabali wake.

Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Uganda anayecheza timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ alisema anafahamu baadhi ya klabu za Tanzania zinahitaji saini yake, hivyo ametoa nafasi kwao kukaa meza moja kuzungumza.

“Kama kuna timu Tanzania zina nia ya kweli, zije mezani tuzungumze,” alisema mshambuliaji huyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz