Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mecky Maxime kurejea Mtibwa ?

Mecky.jpeg Mecky Maxime kurejea Mtibwa ?

Mon, 17 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar umemfuta kazi kocha wake Vicent Barnabas, huku wakitoa sababu mwenendo mbaya wa matokeo licha ya kushinda 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa uliyofanyika jumamosi hii.

Submitted by Tigana Lukinja on Jumatatu , 17th Mei , 2021 kocha Mecky Maxime akitambulishwa Cambiaso Sports Management

Barnabas ambaye ni mchezaji nyota wa zamani wa timu hiyo aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka 15 katika maeneo yote mawili kucheza na kufundisha, ameondolewa kwenye nafasi hiyo aliyoirithi kutoka kwa mchezaji mwenzie wa zamani Zuber Katwila ambaye alijiuzulu.

Mtibwa ambayo ni mabingwa wa ligi kuu mwaka 1999 na 2000 haina mwenendo mzuri kwa taribani misimu mitatu mfululizo, mechi zao za mwisho zimekuwa zinatoa hatma yao,hata msimu wa 2018/2019 ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu shooting ndiyo uliyofanya wakabaki ligi kuu.

Katika mchezo wa jumamosi hii dhidi ya Tanzania Prisons, Mtibwa alikaribisha wachezaji wake nyota wa zamani kuutazama mchezo huu na kutoa ushauri wa ufundi, akiwemo Mecky Mexime,Dua Said , Shaban Ramadhan Omary Kapilima,

Hali inayoweza kutafsiri huwenda kocha ajaye akawa miongoni mwa wachezaji wa zamani kama ilivyokuwa desturi yao.huku Mecky Maxime akitajwa zaidi licha ya kusaini mkataba wa kufanya kazi na kituo cha Cambiaso Sports Management cha Dar-es-Salaam.

Takwimu za Mtibwa katika msimu huu, wamecheza mechi 29 wameshinda 8 wamesare 7 wamepoteza michezo 14 wamefunga magoli 14 na wamefungwa magoli 27 wanadaiwa magoli 13 huku wakiwa na alama 31 katika nafasi ya 14

Chanzo: eatv.tv