Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya Simba vs Prisons yasogezwa mbele tena

13322 Pic+simba TanzaniaWeb

Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Jumatano limetoa taarifa ya kusogezwa mechi ya Simba dhidi ya Prisons ambayo itachezwa saa mbili usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alithibitisha mchezo huo utachezwa saa mbili usiku na sio saa moja kama ambavyo awali ilitangazwa saa moja na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

TIMU ya Simba imerejesha mechi yao Uwanja wa Taifa na kuachana na Uwanja wa Uhuru, ambapo ilitakiwa kushuka dimbani kukipiga na Prisons leo saa kumi jioni lakini mechi hiyo itachezwa saa mbili usiku katika Uwanja wa Taifa.

Kupitia kwa Ofisa wao wa Habari, Haji Manara, alisema wameamua kurejesha mechi hiyo katika uwanja wa Taifa ili kila shabiki wa Simba aweze kupata fursa ya kuangalia mechi hiyo.

“ Mchezo unakuwa siku ya sikukuu kwahiyo ni fursa ya kila shabiki wetu kuhudhuria na ndio maana mechi yetu inachezwa usiku na sio jioni kama ambavyo ilikuwa awali,” alisema.

Akizungumzia wachezaji wa kikosi chao, Cletus Chama na Deogratius Munish ‘Dida’ kuhusu hati zao za uhamisho kuchelewa (ITC), alisema kwamba suala hilo linafatiliwa.

“Kwenye mechi dhidi ya Prison ni ngumu wachezaji hao kucheza, lakini tayari uongozi umeendelea kufatilia masuala yao na tunatarajia kuona mechi zijazo watakuwa katika kikosi chetu,” alisema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz