Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya Simba v TP Mezembe yamalizika kwa suluhu ya 0-0 Taifa

50886 Pic+matokeo

Mon, 8 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Timu ya Simba imetoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya TP Mazembe leo Jumamosi mchezo wa Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hizo  zilitoshana nguvu katika kipindi cha kwanza za mchezo huo. Simba na Mazembe zimecheza mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika na watarudiana Aprili 13 nchini Congo, Lubumbashi.

Katika mchezo huo wote walikuwa wanacheza kwa kuviziana katika kutafuta bao. Hata hivyo Mazembe walikuwa wakishambulia mara kwa mara goli la Simba lakini utulivu wao ulionekana kuwa mdogo katika kuhakikisha wanapata goli la kuongoza.

Kwa upande wa Simba walikuwa wanamtegemea zaidi Meddie Kagere kuwatanguliza mbele hata hivyo naye alikuwa anakutana na ubabe kutoka kwa mabeki wa Mazembe.

Dakika 30 Kagere alitaka kuifungia goli la kuongoza Simba baada ya kubinuka Tiktaka akipokea krosi ya Zana Coulibally na mpira kugonga mwamba kisha ukaambaa na mabeki wa Mazembe kuuondoa haraka.

.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz