Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi nyingine Simba yaahirishwa

Tena Pic Data Mechi nyingine Simba yaahirishwa

Mon, 10 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MCHEZO wa Simba dhidi ya Wagosi wa Kaya Coastal Union uliotarajiwa kupigwa kesho Mei 11, 2021 katika Dimba la Benjamini Mkapa Dar es Salaam umeota mbawa.

Simba inaondoka Dar es Salaam usiku wa kuamkia kesho ikielekea nchini Afrika Kusini ambapo inatarajiwa kumenyana na Kaizer Chief mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi, Mei 15.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ambao ndio wasimamizi wakubwa wa ligi, imesema mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine kutokana na ratiba hiyo ya Simba kusafiri kesho, wakituma barua ya mechi kutokuwepo kwa timu zote mbili.

''Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inapenda kukutaarifu kuwa mchezo tajwa uliopangwa kuchezwa Mei 11 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam umeahirishwa  na utapangiwa tarehe nyingine," imeeleza barua hiyo

Wagosi hao wa Kaya baada ya kuahirishwa kwa mtanange huo sasa nguvu zao wanazielekeza kwa Polisi Tanzania mchezo utakaopigwa Mei 16 katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz