Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi 19, mabao 32 Ligi Kuu Bara

14342 Pic+data TanzaniaWeb

Tue, 28 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya kuchezwa mechi 19 tu katika Ligi Kuu Bara, huku kila timu ikicheza michezo miwili kasoro Yanga na Kagera Sugar pekee zilizocheza mechi mmoja.

Mechi ya Yanga na Kagera Sugar imesogezwa mbele kwa sababu mabingwa mara 27, wapo Rwanda tayari kwa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports.

Katika michezo hiyo 19, mabao yaliyopatikana ni mabao 32 hali ambayo inaonyesha yamepatikana mabao mengi kwa haraka mno katika michezo hiyo.

Timu ambayo imefunga magoli mengi katika michezo yake miwili ni Azam baada ya kuifunga Mbeya City 2-0, Ndanda 3-0 na kuwa jumla ya mabao 5, zikifuatiwa na Simba yenye mabao 3, baada ya kuifunga Prison 1-0 na Mbeya City 2-0,  huku Mbao wao wakiifunga Alliance 1-0 na 1-2 dhidi ya Stand United.

Kwa upande wa timu iliyoruhusu mabao mengi ni Mbeya City, baada ya kufungwa 2-0 na Azam, Simba 2-0, jumla wakiruhusu magoli 4 ikifuatiwa na Mwadui ambayo ilifungwa 2-1 na Kagera Sugar kisha ikafungwa 1-0 na Singida United.

Mabao yaliyopatikana katika michezo yote kwa ujumla, Kagera 2- 1 Mwadui, Singida 0-1 Biashara United, Coastal Union 1-1 Lipuli, Alliance 0-1 Mbao, Ruvu Shooting 0-1 Ndanda, Simba 1-0 Prison, JKT Tanzania 0-0 KMC, Stand Utd 1-0 Afican Lyon, Yanga 2-1 Mtibwa, Azam 2-0 Mbeya City, Coastal Union 1-0 Biashara, Singida Utd 1-0 Mwadui, Ruvu Shooting 1-1 KMC, Stand 1-2 Mbao, JKT Tanzania 1-1 Lipuli, Mtibwa1-0 Prison, Alliance 1-1 Africa Lyon, Simba 2-0 Mbeya City na Azam 3-0 Ndanda.

Chanzo: mwananchi.co.tz