Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchujo ligi kuanza leo

70f7ba4471fae4b8fa20dbec20760e39.png VPL

Fri, 17 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MICHEZO ya mchujo ya kutafuta timu mbili zitakazoungana na Dodoma FC na Gwambina FC kupanda Ligi Kuu inatarajiwa kuchezwa leo katika viwanja tofauti.

Majimaji itacheza na Geita Gold FC katika Uwanja wa Majimaji Songea, Ruvuma na Transit Camp itacheza na Ihefu, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na zitarudiana Julai 22 na mshindi wa jumla atacheza na timu zitakazoshika nafasi ya 15 na 16 kwenye ligi kuu.

Pia Mawenzi Market itaikaribisha Boma FC kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro na Friends Rangers itacheza na Pamba FC katika uwanja ambao utatangazwa baadae na zitaruadiana Julai 21 na washindi wa jumla atakutana na timu za African Sports na Mbuni kutoka daraja la pili.

Julai 25 Mbuni itacheza na mshindi wa jumla kati ya Boma FC na Mawenzi Market katika Uwanja wa Amri Abeid Arusha na African Sports itacheza na mshindi wa jumla kati ya Friends Rangers na Pamba FC katika Uwanja wa Mkwakwani na zitarudiana Julai 30.

Mshindi wa jumla atapanda ligi daraja la kwanza kama itakuwa timu ya daraja la pili na washindwa watashuka daraja la pili kama itakuwa timu ya daraja la kwanza.

Chanzo: habarileo.co.tz