Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezo wa Mwadui vs Njombe Mji wasogezwa kupisha mazishi ya kocha Ntambi

1890 Ntambi TZW

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesogeza mbele kwa siku moja mchezo namba 114 kati ya Mwadui FC ya Shinyanga na Njombe Mji ya Njombe uliokuwa ufanyike Ijumaa Januari 26, 2018 kupisha mazishi ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Mwadui Jumanne Ntambi.



Aliyekuwa kocha msaidizi wa Mwadui FC, Jumanne Ntambi

Mchezo huo sasa utachezwa Jumamosi, Januari 27, 2018.

Kocha huyo msaidizi wa Mwadui alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu kabla ya kufikwa na mauti

Chanzo: bongo5.com