Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchengerwa aipongeza KTO kwa kuanzisha mpira Fursa

WhatsApp Image 2022 02 11 At 8.38.09 PM 1080x640.jpeg Mchengerwa aipongeza KTO kwa kuanzisha mpira Fursa

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: Dar24

Baraza la Michezo nchini (BMT) limepewa mwezi mmoja kuweka mfumo wa kieletroniki kusajili wanachama wake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu ya wanawake yanayojulikana kama Mpira Fursa katika vyuo vya maendeleo (FDCs).

Mashindano hayo ambayo yanaratibiwa na Taasisi ya Karibu  Tanzania Organization (KTO) kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini  (TFF).

“Natoa mwezi mmoja kwa BMT  kusajili taasisi zote za michezo kwa njia ya mtandao, achanen na analogia, usajili ni siku moja,  haiwezekani mtu yupo Ngara mpaka aje physical na bado atatumia siku tatu nne, dunia imebadilika na nyie mbadilike,  mkishindwa kufanya hivyo nitawaondoa, amesema Mchengerwa.

Hata hivyo Waziri Mchengerwa, ameipongeza KTO kwa kuwa na programu ya michezo kwa vyuo vya maendeleo, shule za sekondari na msingi na kwamba itasaidia mkakati wa serikali wa kukuza soka nchi.

“Tunajiandaa kwa miaka nane, atakaetukwamisha tutamtoa, hatuwezi kufanya vizuri kwa kuleana, kila wakati tunaenda tunapigwa  nyundo tatu tunarudi sasa basi, imetosha, serikali ipo tayari kushirikiana na kutoa sapoti yote katika kukuza soka letu  lengo ni kuona tunapiga hatua,”

Mia mjengwa akizungumzia programu ya KTO, amesema KTO inawawezesha wasichana mbalimbali ambao wamekatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ujauzito, mbali na kuwasaidia kujiendeleza katika vyuo vya maendeleo pia wanakuza vipaji vyao katika fan mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu.

Amesema kupitia programu hiyo, imewawezesha wasichana 11 kupata mafunzo ya ukocha chini ya TFF  na wengine 11 wanatarajiwa kuanzia mafunzo hayo.

Chanzo: Dar24