Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbonde anarudi mdogo mdogo Simba

9511 Pic+mbonde TZWeb

Tue, 19 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Beki wa Simba, Salim Mbonde anasema licha ya majeraha ya goti la mguu wa kulia kumsumbua, hajaacha kufanya bidii ya kuzingatia mazoezi anayopewa na daktari.

Mbonde aliumia mzunguko wa kwanza kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar, jambo lililompelekea acheze mechi chache kwa msimu ulioisha.

"Naamini mpaka msimu ujao nitakuwa mtu mwingine baada ya msimu ulioisha kuwa na machungu mengi kwangu, ingawa namshukuru Mungu kwa yote.

"Mazoezi ninayofanya ni kwa mujibu wa daktari anayenitibia, nimekuwa nikifanya bidii inayonisaidia kuanza kuona mwanga wa kupata nafuu, hivyo naamini nitarejea kwenye ubora wangu," anasema Mbonde.

Mbonde anasema anaomba Mungu amjalie afya njema ili aweze kuwa mmoja wa nyota watakaotoa mchango mkubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

Chanzo: mwananchi.co.tz