Dirisha la usajili nchini Uingereza linatarajiwa kufungwa usiku wa leo kabla ya kutimu saa sita kamili, mpaka sasa tetesi za uhamisho kwa baadhi ya klabu kubwa kama Arsenal,Chelsea, Manchester United, Liverpool zikiendelea.
Baada ya takribani siku 30, dirisha la usajili la mwezi Januari hatimaye linafikia tamati usiku wa leo wa siku ya Jumatano huku wadau na wapenzi wa soka kushudia wachezaji watao tua katika klabu zao mpya na wengine kuongeza kandarasi zao.
Klabu ya Chelsea imefanikiwa kukamilisha usajili wa beki, Emerson Palmieri kwa dau la paundi milioni 17.5 akitokea Roma.
Palmieri ameposti picha akiwa na jezi ya timu hiyo hapo jana jioni baada ya kumaliza vipimo vya afya.
Chelsea imeshitushwa na straika, Olivier Giroud kuitumikia timu yake ya Arsenal katika mchezo dhidi Swansea katika kipindi hiki ambacho wapo katika hatua za mwisho za mazungumzo.
Hakuna mikataba yoyote iliyofikiwa lakini Chelsea haikutarajia kumuona Giroud akiingia na kuikabili Swansea lakini inaaminika kuwa ndiyo mchezo wake wa mwisho akiwa na Arsenal . Usajili wake unatarajiwa kufanyika asubuhi ya leo na Chelsea kuweka picha zake majira ya mchana.