Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbio za wanawake kufanyika Machi 7

5fdfdec7925d73cdb8947273359b949f Mbio za wanawake kufanyika Machi 7

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WANAWAKE wa rika mbalimbali wamehimizwa kujitokeza na kujisajili kwa ajili ya ushiriki wa mbio za wanawake zitakazofanyika Machi 7, mwaka huu.

Akizungumzia mbio hizo zinazofahamika kama Mbio za Wanawake Tanzania muandaaji Pili Amir alisema lengo ni kutengeneza jukwaa la wanawake wa rika tofauti kukutana na kujadili uzoefu, changamoto na kujifunza ushiriki wao katika kukuza uchumi wa nchi.

“Tunataka pia kuunga mkono harakati za Rais John Magufuli kukuza uchumi wa wanawake na watanzania na kuchukua tahadhari ya kujikinga na magonjwa mbalimbali kupitia mazoezi ya viungo ikijumuisha na kukimbia kwa afya,”alisema.

Alisema mbio hizo zitakuwa za km 5, 2.5 kwa watoto na km 10 ambapo washindi watapewa medali na zawadi mbalimbali kutoka kwa wadhamini wao wakuu GSM. Aliongeza kuwa gharama za usajili ni sh. 35,000 kwa njia ya mtandao.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Smart Deus alisema wameamua kudhamini mbio hizo kutambua mchango wa wanawake na kwamba watatoa asilimia 15 ya punguzo za bei zao kwa ajili ya washiriki wote.

Naye muwakilishi wa Bakhresa Group kupitia Azam Media Yvonne Cherrie ‘Monalisa’ alisema wao wamejipanga kurusha mbio hizo kupitia televisheni ambapo pia, watatoa maji ya Uhai kwa washiriki.

“Mbio hizi ziwe chachu kwa wanawake kufanya mazoezi na kulinda afya zao,”alisema msanii huyo wa filamu.

Chanzo: habarileo.co.tz