Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbio za magari zawaza mashabiki

RARRY.webp Mbio za magari zawaza mashabiki

Fri, 29 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHAMA cha Mbio za Magari Tanzania (AAT), kimesema kimekamilisha kuandaa programu zake na kiko tayari kukutana na viongozi wa Baraza la Michezo Nchini (BMT), ili kujadiliana na kupanga mikakati.

BMT imevitaka vyama vyote vya michezo kuwasilisha programu zake kwa ajili ya kutoa mwongozo wa utekelezaji wake katika kipindi hiki cha janga la corona.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa AAT, Athuman Khamis, alisema wanatarajia kikao hicho kitasaidia kufanyika kwa mashindano yao baada ya viongozi wa chama kukutana na kujadiliana kwanza.

"Mchezo wetu unakusanya watu wengi, lazima tukubaliane na wito huo wa serikali juu ya kupeleka programu na mikakati yetu, hii itatusaidia kupata ufafanuzi juu ya kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya corona," Khamisi alisema.

Aliongeza endapo mchezo huo utarejea bila ya kuhusisha mashabiki, kwao itakuwa ni changamoto na hasa kwa upande wa kiuchumi.

"Tunasubiri agizo la serikali, suala la kutokuwa mashabiki kwetu ni mtihani, sisi tunapata pesa kwa wale wanaokuja kushuhudia mashindano yetu ili kusaidia chama na shughuli nyingine, kiuchumi tutayumba," aliongeza kiongozi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live