Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbio za magari mambo magumu

Thu, 7 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHAMA cha Mbio za Magari Tanzania (AAT), kimesema endapo serikali itaruhusu michezo kurejea bila mashabiki, kwa upande wao watakuwa na wakati mgumu kwa sababu wataathirika kiuchumi.

Akizungumza na gazeti hili, Msemaji wa AAT, Athuman Khamis alisema wamesikia kauli ya Rais John Pombe Magufuli juu ya kufikiria kurejesha Ligi Kuu, lakini bado hawana uhakika kama michezo itarejea kama ilivyokuwa awali.

Khamis alisema endapo watarejea katika michezo bila kuruhusu mashabiki, kwao watakuwa na changamoto kwa sababu mashindano yao hufanyika kwa kutegemea wadhamini.

"Tunasubiri mwongozo wa serikali, suala la kutokuwa na mashabiki kwetu ni mtihani, sisi tunapata pesa kwa wale wanaokuja kushuhudia mashindano yetu, ili kusaidia chama kupata fedha za kujiendesha," alisema Khamis.

Alisema endapo utachukuliwa uamuzi wa kutoruhusu mashabiki, AAT italazimika kukutana kujadili hatima ya michuano inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live