Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbinu za ushindi Yanga, Azam CAF

77587 YANGA+PIC

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Yanga na Azam zitakuwa ugenini leo zikifanya uamuzi wa kuendelea ama kuaga mashindano ya kimataifa wakati zitakapocheza mechi zao za marudiano katika viwanja vya ugenini zikibeba matokeo yasiyoridhisha ya mechi za mkondo wa kwanza.

Watoto wa Jangwani, Yanga ambao walibanwa kwa sare ya 1-1 dhidi ya Zesco katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika jijini Dar es Salaam, watakuwa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola kuwakabili mabingwa hao wa Zambia, wakati Azam waliolala 1-0 nyumbani dhidi ya Triangle, watajaribu kupindua meza ugenini Zimbabwe katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amesema alisema wako tayari kupambana na Zesco leo na wataingia na hamasa ya hali ya juu.

“Tupo tayari kwa mchezo na wachezaji wote wana morali ya juu. Tunawaheshimu Zesco tunatambua kuwa wako nyumbani na wana rekodi nzuri wakiwa hapa lakini tumekuja na malengo yetu, tunaamini mchezo utakuwa mzuri na kubwa tunaamini tuna nafasi ya kutinga hatua ya makundi,” alisema Mwandila.

Katika mazoezi ya mwisho, Zahera alikuwa akihangaika kutafuta beki wa kulia mbadala wa Paul Godfrey ‘Boxer aliye majeruhi na alikuwa akiwapima Ally Ally na Juma Abdul ingawa Abdul ana nafasi kubwa ya kuanza leo.

Yanga itapaswa kuepuka kutegemea mbinu moja kuikabili Zesco United na badala yake wanahitajika kuingia uwanjani wakiwa na mipango mbadala ya kuwabana wapinzani hao ambao hubadilika kulingana na mchezo.

Pia Soma

Advertisement
Zesco United wamekuwa ni wajanja wa kubadilika haraka pindi wanapogundua uimara na udhaifu wa wapinzani jambo linaloweza kuigharimu Yanga ikiwa benchi lake la ufundi halitojipanga nalo.

Katika mchezo wa kwanza, Yanga walijaza idadi kubwa ya wachezaji kwenye safu ya kiungo wakiwa na lengo la kudhibiti mbinu ya Zesco kushambulia kupitia katikati lakini baada ya kuona mpango wao umeshtukiwa Wazambia hao walibadilika na kuanza kuufungua uwanja na kushambulia kupitia pembeni jambo ambalo liliwapatia bao.

Kocha wa Zesco, George Lwandamina ‘Chicken’ alibainisha namna alivyombadili mara tatu nafasi za kucheza kiungo Thaban Kamusoko katika dakika za mwisho za mchezo wao wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa kabla ya nyota huyo wa zamani wa Yanga kuwadungua waajiri wake wa zamani kwa bao la dakika ya mwisho.

Lakini pia ni mechi ambayo Yanga wanapaswa kucheza kwa nidhamu kubwa na kiujumla kutumia zaidi mashambulizi ya kushtukiza ili kutengeneza uimara zaidi kwenye safu yake ya ulinzi ambayo haipaswi kuruhusu mabao ambayo yanaweza kuwagharimu.

Zesco ni timu ambayo imekuwa ikijilipua kwa kushambulia zaidi pindi inapokuwa nyumbani na hivyo kitendo cha Yanga kulazimisha kupishana nao kinaweza kufungua mianya ambayo wapinzani wao wanaweza kuitumia kuwaadhibu.

Ikumbukwe kwamba licha ya kutofunga bao kwenye mechi iliyopita jijini Dar es Salaam, washambuliaji wa Zesco United, Jesse Were, Winston Kalengo na Umaru Kasumba bado ni tishio kwa Yanga kwenye mechi hiyo ya marudiano.

Raia wa Kenya, Were wiki iliyopita amefunga mabao manne katika mechi mbili mfululizo ambazo Zesco United imecheza kwenye Ligi Kuu ya Zambia dhidi ya timu za Nakambala Leopards na Lumwana Radiants.

Kingine ambacho kinaweza kuisaidia Yanga kwenye mchezo huo ni wachezaji wake hasa wale wanaocheza kwenye safu ya ushambuliaji na kiungo kufika haraka na kwa idadi kubwa kwenye eneo la hatari la wapinzani wao pindi wanapokuwa wanashambulia.

Azam sasa

Azam itacheza na Triangle FC ya Zimbabwe leo lakini ikiwa na kazi mbili, kwanza kupata ushindi ili isonge mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, lakini jambo la pili ni kuanza kufuta rekodi mbovu katika mechi zake za ugenini.

Kujituma bila ya kukata tamaa, kujilinda kwa nidhamu, kushambulia kwa tahadhari na umakini katika lango la wapinzani vitaisaidia Azam kupindua meza ugenini leo baada ya kutawala mchezo wa kwanza nyumbani, kisha kuruhusu kipigo cha goli 1-0.

Chanzo: mwananchi.co.tz