Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya kwanza, ya kwanza kupanda ligi kuu

Mbeya Kwanza Mbeya kwanza, ya kwanza kupanda ligi kuu

Sun, 25 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Timu ya soka ya Mbeya kwanza kutoka Mbeya, imekuwa timu ya kwanza kupanda ligi kuu msimu ujao ya 2021/2022 ikiwa imesalia mechi 3.

Mbeya kwanza iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Sports katika uwanja wa Mabatini Mlandizi Pwani na kujikusanyia alama 38 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yeyote kwenye kundi A.

Timu hiyo inayofundishwa na Steven Matata akisaidiwa na Michael Mnyali maarufu kama 'Chuji' imefanikiwa kupanda baada ya kucheza daraja hilo kwa misimu kadhaa bila mafaniki, ikiwemo kuhama viwanja vya nyumbani kuna wakati walitumia Sokoine Mbeya kisha CCM Mkwakwani na baadaye Mabatini Mlandizi ambapo ndipo walipo kupandia.

Meneja wa timu hiyo nyota wa zamani wa Nazareth,Simba na Timu ya Taifa Emanuel Gabriel 'Batgol' hakusita kuonesha furaha yake alisema'' najiona kama mwenye bahati miaka 20 iliyopita niliipandisha Nazareth ya Njombe maarufu kama 'watoto wa Baba Paroko' nikiwa mchezaji, leo hii baada ya miaka 20 nafurahi kuipandisha Mbeya kwanza nikiwa meneja''

Timu hiyo iliyokuwa na wachezaji wazoefu na chipukizi kama David Naftal aliyoichezea Simba timu ya Taifa na miaka kadhaa nyuma kabla ya kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Kenya na Zambia, imemaliza kundi wakiwa na alama 38 wakifuatiwa na Africa Sports 28 huku michezo iliyobaki kwa kila timu ni 3 tu

Shughuli pevu ipo kwenye kundi B ambalo zaidi ya timu tatu zina alama zinazokaribia, kundi linaongozwa na Geita Gold wenye alama 28 kwenye michezo 12, Pamba ya Mwanza na Kitayosa zenye alama 27 kila moja zikiwa zimebakiza michezo 6 kumaliza msimu

ligi hiyo yenye timu 20 kutoka makundi mawili yenye timu 10 kila moja, kinara 1 wa kila timu itapanda ligi kuu moja kwa moja na wale watakaoshika nafasi ya pili na wa tatu watacheza mechi za mtoano 'play off'' na timu za ligi kuu zilizoshika nafasi ya 13 na 14

Chanzo: eatv.tv