Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City Wagoma Kushuka Daraja Ligi Kuu Bara

Simba Sc Captain John Bocco Vs Mbeya City 4anfdrievhqd13ccm0f5iy3ku?fit=1200%2C800&ssl=1 Mbeya City Wagoma Kushuka Daraja Ligi Kuu Bara

Fri, 9 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mbeya City Wagoma Kushuka Daraja Ligi Kuu Bara July 9, 2021 by Global Publishers



MENEJA wa Timu ya Mbeya City, Mwegane Yeya, amesema kikosi hicho kinapambana kuhakikisha kinaibuka na ushindi kwenye mechi mbili zilizobaki kwenye Ligi Kuu Bara ambazo ni sawa na dakika 180.

Mbeya City inapambana kujinasua na janga la kushuka daraja ambapo inahitaji pointi sita ili kufufua matumaini ya kubaki kwenye ligi. Tayari kikosi hicho kimekusanya pointi 36 kwenye mechi 32.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwegane alifunguka kwamba: “Tumebakiwa na mechi mbili kumaliza ligi dhidi ya Gwambina na Biashara United, ni mechi ambazo tutamaliza nyumbani, hivyo ni lazima tupambane kuhakikisha tunapata matokeo mazuri ili tujihakikishie nafasi ya kubaki kwenye ligi.

“Hatupo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo, hivyo tutapambana kwa jasho na damu kwenye mechi hizi ili tuwe sehemu salama.”

Mbeya City inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36 baada ya kushuka dimbani mara 32, imeshinda mechi nane, sare 12 na kupoteza 12.

STORI: HUSSEIN MSOLEKA, Dar es Salaam

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz