Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbelgiji atuliza mizuka Msimbazi

11828 Pic+mbelgig TanzaniaWeb

Tue, 14 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Sare ya bao 1-1 ya Simba dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na suluhu dhidi ya Namungo FC ya Daraja la Kwanza kwenye uzinduzi wa Uwanja wa Majaliwa, Lindi umeshtua mashabiki wa timu hiyo.

Lakini kocha wake, Patrick Aussems amewaambia: “Acheni presha ninyi, msiziangalie kabisa Kotoko na Namungo FC, mimi ndiye nilikuwa ninaangalia…kuna kitu nilikuwa nafuatilia na nimekipata, sikuwa kwa ajili ya matokeo.”

Sare na suluhu hizo zimekuja ikiwa ni siku chache baada ya Simba kutoka Uturuki ilikokuwa imeweka kambi ya wiki mbili huku ikielezwa kuwa imeiva kila idara na kila atakayegusa, atakiona cha moto.

Kauli ya Aussems

Aussems alisema kwamba kwa upande wake hana mpango na matokeo ya ushindi katika mechi yoyote ile kati ya hizi za kirafiki ila kuna mambo ambayo alikuwa anangalia.

“Nilikuwa ninaangalia viwango vya kila mchezaji katika ubora wake wa kukaba na kushambulia na kuona kama wanatimiza yale ambayo nilikuwa nikiwapatia katika mazoezi yote ambayo wamefanya.

“Tumefanya mazoezi magumu nchini Uturuki na nilichokua ninaangalia ni jinsi gani tunacheza na kujua kila mchezaji wangu ana ubora upi na upungufu ili kumrekebisha kabla ya msimu wa kimshindano kuanza.

“Ninadhani mara baada ya kucheza mechi ya mwisho ya kirafiki na hapo ndio nitakuwa ninafahamu kila kitu katika timu haswa viwango vya wachezaji na tutakwenda katika mechi ya Mtibwa tukiwa na akili ya kupata ushindi tu.

Simba kabla ya kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo itakuwa Agosti 18 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza watacheza mechi ya mwisho ya kirafiki Agosti 15 dhidi ya Arusha United jijini Arusha na baada ya hapo watakwea pia kwenda Mwanza.

“Naomba wapenzi wa Simba wote watulie kwani ushindi utaanza katika mechi za mashindano na nina imani timu itafanya hivyo lakini hizi mechi za kirafiki ni kama majaribio tu kwangu,” alisema Aussems .

Mtibwa waikamia Simba

Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila ameiangalia Simba kuelekea kwenye mchezo wa Jumamosi wa Ngao ya Jamii na kusema haitishi hata kidogo licha kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki na kusema lazima wakae.

“Hakuna ambacho Simba imebadilika, ingawa imekwenda Uturuki kuweka kambi lakini iko vile vile, haijawa na kiwango cha timu za kiarabu na hata ingekuwa na kiwango hicho bado tungeifunga tu, wala haitupi presha,” alisema kocha Katwila katika mahojiano maalumu na gazeti hili.

Alisema kikosi cha Mtibwa Sugar kitaondoka Morogoro keshokutwa Alhamisi kwa basi kwenda Mwanza tayari kwa mchezo huo.

“Yote hayo sio kitu kwetu, narudia tena sijaiona tofauti na Simba ya Uturuki na ile ya siku zote ya Msimbazi tuliyoizoea, sioni ilichobadilika hata baada ya kurejea kutoka kambini Uturuki,” alisema kocha Katwila kwa kujiamini.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake, kocha huyo alisema wanachokisuburi hivi sasa ni siku ya mechi tu na si vinginevyo.

“Maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo tulishamaliza, hivi sasa tunafanya mazoezi mepesi tukisubiri mechi, wachezaji wote wako vizuri si kimwili hata saiokolojia ya kila mmoja iko vizuri kwa ajili ya mchezo huo,” alisema.

Katwila anasema mipango yao ni kuifunga Simba Jumamosi, kitu ambacho kinawezekana licha ya kukataa kuelezea mapungufu ya wapinzani wao na mbinu anayodhani itamuwezesha kutwaa ushindi zaidi ya kusisitiza ushindi utakwenda Mtibwa.

Mtazamo

Mchambuzi wa Soka nchini, Ally Mayay alisema mechi hiyo itakuwa nusu kwa nusu kwa timu zote na mshindi ataamuliwa na mbinu za makocha. “Vikosi vyote viko sawa japo katika maandalizi na Simba ni bora zaidi kuanzia kambi ya Uturuki na hata usajili wao, Mtibwa kama ilivyo sera ya klabu yao, haijawahi kuwa na tatizo la wachezaji hata kama itabomolewa.

“Kitakachowabeba Mtibwa ni uwezo wa kupambana kwa pamoja kitimu, ushirikiano na mbinu za kocha, upande wa Simba ni uwezo wa mchezaji mmoja mmoja,” alisema Mayay.

Chanzo: mwananchi.co.tz