Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbelgiji Sven afumua usajili Simba SC

91357 Sven+pic Mbelgiji Sven afumua usajili Simba SC

Fri, 10 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

SIMBA chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroek haijapoteza mechi yoyote mpaka sasa zaidi ya sare ya 2-2 dhidi ya Yanga, lakini unaambiwa baada ya kuwasoma nyota wake kocha huyo amepanga kufumua usajili wake ili kujenga kikosi imara zaidi. Katika kukisuka zaidi Simba iwe katika ubora anaoutaka Sven ameanza msako wa mashine mbili mpya kimyakimya. Mabosi wa Simba walimsajili winga wa UD Songo Luis Jos Miquissone katika kuisuka zaidi safu hiyo ya ushambuliaji lakini bado Sven ametaka straika mmoja zaidi. Taarifa za uhakika ambazo Mwanaspoti limezipata ni kwamba, Kocha Sven ameingia kazini mwenyewe kusaka straika mpya, huku akiendelea kumwangalia na kumsuka nahodha wake John Bocco ambaye amerejea kazini akitoka katika majeruhi ya muda mrefu. Mbali na straika wa kati pia kocha huyo anataka kusajili beki wa kati mwingine mkali mwenye sifa kama Ally Mtoni ‘Sonso’ anayekipiga Yanga kwani tayari ameonyesha kutokubaliana sana na baadhi ya mabeki wake wa kati waliopo. Kocha huyo ameingia katika msako wa kutafuta beki wa kati anayeweza kutumia mguu wa kushoto na kama atafanikiwa kumpata kabla dirisha dogo halijafungwa Januari 15, wakongwe waliopo kikosini, Erasto Nyoni au Pascal Wawa mmoja wao anaweza kupoteza nafasi kabisa. Habari za chini ya kapeti zinasema, Sven hajamkubali Nyoni licha ya mabosi wa klabu hiyo kumkingia kifua wakidai hakuna beki bora wa kati kama yeye nchini’. Lakini inaelezwa, anachokitaka Kocha Sven ni kuwa na beki wa namna hiyo ili aweze kuwa katika ubora wa kusaidia beki ya kushoto ambayo bado anaona kuna makosa yanatokea upande huo. Maana halisi anachotaka Sven ni kuwa na ukuta wa sasa kama wa Yanga ambao wanamtumia mabeki Kelvin Yondani anayecheza sambamba na Ally Mtoni Sonso. Mtu kama Sonso ndiye anamtaka Sven ambapo atakuwa na ubora wa kukabiliana na mazingira yoyote ya mapungufu kutoka upande wa beki wa kushoto wa timu yake. Hata hivyo, Sven atakabiliana na ugumu katika kupata beki wa namna hiyo ambao ni adimu katika soka ambao wana ubora mkubwa, huku ikielezwa chaguo lake lipo zaidi nje ya nchi. Yanga iliwahi kuyumba kutafuta beki wa namna hiyo enzi za Kocha Mzambia George Lwandamina na hakupata. Kuna uhakika kwamba usajili huo ukikamilika baadhi ya mabeki wa kati wanaweza kuondoka haraka kutokana na kuwa katika nafasi ngumu ya kuweza kupata nafasi. Kocha huyo kesho atakiongoza kikosi chake kwenye pambano la nusu fainali dhidi ya Azam FC katika mfululizo wa michuano ya Kombe la Mapinduzi 2020, ikiwa ni mechi yake ya Simba tangu achukue nafasi ya Patrick Aussems, nne zikiwa za Ligi Kuu Bara, moja ya Kombe la FA na moja ya Mapinduzi dhidi ya Zimamoto.

Chanzo: mwananchi.co.tz