Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaraka Yusuf mdogo mdogo

69070 Mbaraka+picha

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BAADA ya kuwa nje kwa muda mrefu, straika nyota wa zamani wa Kagera Sugar, Mbaraka Yusuf ameanza mazoezi mepesi kuonyesha anajiandaa kurejea uwanjani, japo hataweza kucheza kwenye duru la kwanza la Ligi Kuu akiwa Azam yenye mkataba naye.

Nyota huyo aliyekuwa aikiichezea Namungo FC kwa mkopo, amesharejeshwa klabu yake ya Azam baada ya kuumia wakati akiipigania timu hiyo ya Lindi kupanda Ligi Kuu kwa msimu ujao.

Mbaraka ameliambia Mwanaspoti kwa namna anavyoendelea anaamini mpaka raundi ya pili anaweza akarejea uwanjani kuendelea na kazi yake.

Amesema kazi ya soka ina changamoto zake kama kuumia jambo alilodai awali lilikuwa linamuumiza kichwa lakini kwa sasa amekubali hali badala yake anapambana kuhakikisha anazingatia mazoezi kwa mujibu wa daktari anayemsimamia.

"Naendelea vizuri tofauti na mwanzo kwa sasa nafanya mazoezi mepesi kwa raundi ya kwanza itakuwa ngumu kabisa kucheza nitakuwa bado sijatengemaa, ila raundi ya pili nitaanza kazi Mungu akipenda," amesema na kuongeza;

"Soka ni kazi yangu hivyo sio kitu rahisi kukaa nyumbani bila kufanya kazi ila mwisho wa siku lazima saikolojia yangu ikubali kwamba ndio changamoto za kazi zetu,"anasema.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz