Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbao yaivua ubingwa Gor Mahia ikiifunga penalti 4-3

38118 Pic+mbao Mbao yaivua ubingwa Gor Mahia ikiifunga penalti 4-3

Wed, 23 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbao imetinga nusu fainali ya mashindano ya SportPesa baada ya kuwafunga Mabingwa watetezi Gor Mahia ya Kenya kwa  penalti 4-3. Ikishangiliwa uwanja mzima na mashabiki wa Simba na Yanga,Mbao ilionyesha kandanda safi hasa kipindi cha pili na kuwabana vilivyo wapinzani wao. Timu hizo zilikwenda hatua ya penalti baada ya dakika 90 kutoka sare ya bao 1-1. GorMahia ndio ilikuwa ya kwanza kufunga bao dakika ya 52  lililofungwa kwa Penalti na Dennis Oliech kabla ya Mbao kusawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Raphael Siame. Mbao iliendelea kufanya mashambulizi lakini safu ya ulinzi ya Gor Mahia ilikuwa makini kuokoa hatari zote langoni kwao. Katika mikwaju ya penalti, Gor Mahia walifunga kupitia kwa Francis Kahata, JacquesTuyisenge ,na Boniface Omond wakati Harun Shakavah na Shafik Batambuze walikosa. Mbao ilifunga penalti zao kupitia kwa Said Khamis,Raphael Siame, Hamimu Abdukarim na David Mwasa wakati Hashimu Ibrahim alikosa.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz