Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbao FC wajipanga kukoleza safari African Lyon

56289 Pic+mbao

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MWANZA.MBAO FC kesho Alhamisi watawavaa vibonde wa Ligi Kuu African Lyon lakini Kocha Msaidizi wa kikosi hicho Fulgence Novatus amesema hakuna kingine kitakachowafanya wawe salama zaidi ya kupata ushindi katika mtanange huo.

Kikosi hicho chenye maskani yake eneo la Sabasaba jijini hapa mpaka sasa kina pointi 40 wakiwa katika nafasi ya 13 katika Msimamo wa Ligi hiyo.

Ushindi wowote wa Mbao FC katika mpambano huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Uhuru utawaweka angalau katika nafasi nzuri ya kubaki kwenye Ligi hiyo msimu ujao.

Akizungumza na Mwanaspoti,Novatus alisema mchezo huo wanauchukulia kwa umakini mkubwa kwani wakipata pointi tatu zitawafanya wawe katika nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu.

Alisema kamwe hawatowadharau African Lyon katika mchezo huo licha ya kuwa vibonde hivyo wataingia kamili kusaka ushindi.

“Tutamkosa Mshambuliaji wetu Ndaki Robert ambaye amepata jeraha la enka lakini nafasi yake tayari imeshapata mtu wa kucheza hivyo kikubwa ni ushindi katika huu mchezo”alisema Novatus.

Kocha huyo alisema ushindi walioupata wa bao 1-0  katika mchezo wao na Ndanda FC umewapa nguvu kubwa wachezaji wao ambao wamepata morali katika mapambano ya kuibakisha timu hiyo Daraja.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz