Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele aitanguliza Yanga Dakika 45 za kwanza

MAYELE FISTON ayele aitanguliza Yanga Dakika 45 za kwanza

Sun, 10 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

PAMOJA na Yanga kupata bao 1-0 kipindi cha kwanza kocha anakazi kubwa ya kufanya kuhakikisha kikosi chake kinapata mabao mengi kutokana na nafasi wanazotengeneza.

Bao la yanga limefungwa dakika ya 43 na mshambuliaji Fiston Mayele akipokea pasi safi kutoka kwa David Brayson.

Baada ya bao hilo Yanga waliamka na kuliandama lango la JKU dakika ya 44 Mayele nusula awainue tena mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kidogo kuisapoti timu yao baada ya kuchongewa krosi na Brayson na kichwa chake kutoka nje kidogo ya pango.

Yanga wameanza vizuri kipindi cha kwanza kwa kuliandama mala kwa mala lango la JKU ambao pia umakini wao umechangia kupunguza idadi ya mabao kipindi cha kwanza.

Kwa upande wa Yanga ambao kocha Nabi amewaanzisha nyota wake wengi ambao hawana nafasi kikosi cha kwanza wanakazi kubwa kuhakikisha wanapata nafasi kikosi cha kwanza kutokana na makosa mengi wanayoyafanya.

Kwa upande wa wapinzani JKU wameonekana kuwa vizuri eneo la ulinzi huku safu yao ya ushambuliaji ikitawaliwa na washambuliaji ambao wanachezua sana mpira wakipata nafasi.

Wakati safu ya ulinzi iliongozwa na Yanick Bangala, Abdalah Shaib, David Brayson na Paul Godfrey wakeonekana kucheza vizuri kwa kuelewana.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz