Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele aanza kazi ya mabao Yanga

Fiston Mayele aanza kazi ya mabao Yanga

Sat, 4 Sep 2021 Chanzo: ippmedia.com

Yanga ambayo iliweka kambi nchini Morocco, imecheza mechi moja tu kubwa ya kirafiki dhidi ya Zanaco FC ya Zambia na kufungwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Siku ya Kilele cha Mwanachi.

Hata hivyo, juzi ilicheza mechi ya ndani ya mazoezi dhidi ya Friends Ranger FC ya Manzese, Dar es Salaam na kushinda kwa mabao 3-1, shukrani zikimwendea Fiston Mayele, Ditram Nchimbi na Yusuph Athuman, waliocheka na nyavu.

Mayele ni moja ya usajili mpya wa timu hiyo katika nafasi ya ushambuliaji, na mashabiki wa timu hiyo walikuwa na kiu ya kutaka kumuona akicheka na nyavu kwenye mechi dhidi ya Zanaco lakini hakufanikiwa kuliona lango.

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, aliliambia gazeti hili kuwa bado anahitaji kupata mchezo mmoja mkubwa wa kirafiki kabla ya kuikaribisha Rivers United ili kuona kama wachezaji wake wanaweza kukihamisha kile anachowafundisha mazoezini kwenye mechi.

Hata hivyo, mapema wiki hii, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela, alisema uongozi upo katika mipango ya kutafuta mechi hiyo ili kukidhi matakwa ya kocha kabla ya kuwavaa Wanaigeria hao.

Kikosi cha Yanga kinaundwa na nyota wengi wapya waliosajiliwa dirisha hili, hivyo kocha Nabi amesema bado hajapata muunganiko mzuri wakati huu ratiba ya michuano ya kimataifa ikianza mapema kabla ya Ligi Kuu Bara.

Chanzo: ippmedia.com