Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele, Fei Toto watupia Yanga yapanda kileleni

FISTON MAYELE Mayele, Fei Toto watupia Yanga yapanda kileleni

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Songea. Yanga imejihakikishia pointi tatu ugenini baada ya kuilaza KMC mabao 2-0 na kuibuka na ushindi katika uwanja wa majimaji Songea.

Ushindi huo unawafanya Yanga wakae kileleni mwa ligi na jumla ya point 9 baada ya michezo mitatu na ushindi wa ikiwa wa idadi kubwa ya mabao tangu ligi ianze.

Katika mchezo huo wana Jangwani walionekana kuwa na uchu zaidi wa mabao kutokana na kuanza kwa kasi na kufanikiwa kupata mabao ya haraka kupitia kwa Mayele dakika ya nne na Feisali Salum dakika ya 10, mabao ambayo yalidumu hadi dakika 90 za mchezo kukamilika.

Hata hivyo timu zote zilifanya mabadiliko, ambapo, KMC iliwatoa Awesu Awesu, Miraji Athuman na Hassan Kabunda, Abdul Hilali na nafasi zao kuchukuliwa na Idd Kipagwile, Matheo Anthony, Mohamed Samata na Charles Ilanfya.

Yanga wao waliwatoa Mayele, Moloko Jesus, Bangala na nafasi zao kuchukuliwa na Yusuph Athuman na Heritier Makambo na Mauya.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz