Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxime afurahia kuanza vema

13958 Maxme+pic TanzaniaWeb

Mon, 27 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya msimu uliopita kuwa na mwanzo mbaya wa mechi za Ligi Kuu, ukiwa ni msimu wake wa kwanza akiwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amecheka mwanzo mzuri alioupata msimu huu. Maxime ambaye msimu uliopita hakupata matokeo katika mechi kadhaa za mwanzoni mwa msimu na kudhaniwa angekuwa mmoja wa makocha ambao wangetimuliwa mapema, msimu huu kwake umekuwa mtamu.

Juzi aliiongoza Kagera Sugar kuibuka na ushindi ikiwafunga wageni wao Mwadui FC mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Katika mchezo huo wenyeji walitoka nyuma na kuibuka na ushindi uliompa tabasamu Maxime ambaye anasema kama sio kujituma kwa vijana wake mambo yangewaendea kombo.

Aidha ushindi huo umeifanya timu hiyo kuendelea kuitambia Mwadui kila zinapokutana wenye Uwanja wa Kaitaba, kwani tangu ipande daraja mwaka 2015 haijawahi kupata ushindi dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja huo, ilishafungwa 1-0,1-0, 2-0 kabla ya juzi kufungwa 2-1.

Maxime alisema licha ya kupata ushindi lakini wapinzani wao walicheza vema kwa muda wote wa mchezo hivyo kuufanya mchezo huo kuwa mgumu.

“Hakuna kitu kizuri kama kuanza ligi kwa ushindi, msimu uliopita tulijikuta kwenye wakati mgumu na shinikizo zito kwa kuanza vibaya, safari hii wachezaji wangu wamepambana vya kutosha sio jambo rahisi kutoka nyuma na baadaye kupata ushindi.

Chanzo: mwananchi.co.tz