Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matola asaini mwaka mmoja Polisi Tanzania

62706 Pic+matola

Sat, 15 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BAADA ya kufanikiwa kupanda Ligi Kuu Bara, uongozi wa Polisi Tanzania FC, umemsainisha mkataba wa mwaka mmoja, Suleiman Matola kuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Charles Mkumbo alisema wameamua kumchukua Matola kutokana na kuwa na historia nzuri kwenye soka la Tanzania tangu akiwa mchezaji na hata kwenye nafasi ya ukocha.

"Kila mmoja anafurahia utendaji kazi wa Matola, hilo ndilo limetusukuma kumtafuta na kumpa kazi, hivyo baada ya mwaka mmoja kama ataridhika kuendelea kufanya kazi na sisi au pande zote zitafurahishwa basi tutaendelea kuwa naye ila kwa sasa tutakuwa naye kwa mwaka mmoja," anasema Mkumbo.

Aliongeza suala la usajili litakuwa juu yake na watatimiza mapendekezo atakayoyaleta kwa uongozi ili kumnasa mchezaji yoyote atakayempendekeza.

"Hatupendi kusikia ameingiliwa kwenye suala la usajili, ndio maana kazi hiyo itabaki kwake na benchi la ufundi katika kutimiza malengo ya timu."

Hata hivyo Matola alisema falsafa yake haitabalidilika kwa kuwapa kipaumbele wachezaji wazawa kuliko wageni kutokana na mfumo wa soka la Tanzania lilivyo.

"Nilipokuwa Lipuli FC wachezaji wangu walitoka hapa nchini, hivyo hakuna mabadiliko kwenye hilo ndio maana tunahitaji kuanza kazi mapema ya kuwaweka wachezaji pamoja kabla ya ligi kuanza," anasema Matola

Polisi katika kuimarisha benchi la ufundi wamemteua kocha Ali Suleiman Mtuli kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.

Timu hiyo imepanda TPL sambamba na Namungo FC baada ya kufanya vyema kwenye Ligi Daraja la Kwanza (FDL) iliyomalizaka mwezi uliopita ikiwa na Pointi 47 chini ya Kocha Mbwana Makata aliyemaliza muda wake.

Chanzo: mwananchi.co.tz