Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matajiri wapya Newcastle wataka mataji

Newcastle Matajiri wapya Newcastle wataka mataji

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

WAMILIKI wapya wa klabu ya Newcastle United wamesema wanataka kuibadili na kuwa timu kubwa kama Manchester City na Paris Saint-Germain, baada ya kukamilisha kuinunua kwa Pauni milioni 305.

Mmiliki mwenza wa klabu hiyo, Amanda Staveley ameelezea matarajio ya ushirika wao unaosaidiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF).

Newcastle maarufu 'Magpies' sasa inakuwa klabu yenye wamiliki matajiri zaidi duniani.

Akizungumza na maelfu ya mashabiki waliokuwa wakishangilia makao makuu ya klabu hiyo pale St James' Park, Staveley alisema:"Tunataka kuona mataji. Laki mataji yanahitaji uwekezaji, muda, subira na ushirikiano."

Wamiliki hao wamependekeza Kocha wa sasa wa Leicester City, Brendan Rodgers kuwa mwalimu mpya wa Newcastle.

Chanzo: ippmedia.com