Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maswali 10 yenye utata mechi Simba, Yanga

Maswali Pic Data Maswali 10 yenye utata mechi Simba, Yanga

Mon, 10 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

PAMBANO la watani wa jadi, Simba na Yanga juzi lilishindwa kufanyika baada ya mkanganyiko wa mabadiliko ya muda wa kuanza kwa mchezo. Uamuzi huo umeibua maswali 10 tata...ebu yasome...

1. Barua au waraka rasmi wa kusogeza muda wa mchezo ulitumwa muda gani, kutoka wapi na ulikuwa na sababu zipi?

2. Je, TFF na Bodi ya Ligi (TPLB) iliishauri kipi taasisi husika iliyotaka kusogeza mbele muda wa mchezo kulingana na kanuni za soka?

3. Kama hoja ni kudaiwa kuwa na ugeni wa Kitaifa unaokuja uwanjani kwani haijawahi kutokea ugeni wa namna hiyo kufika wakati mchezo ukiwa umeshaanza?

4. Je,taarifa ya kusogezwa mbele kwa muda wa kuanza mchezo ulizifikia klabu wakati gani?

5. Nini hatma ya fedha za mashabiki waliokuwa waungwana kwa kukata tiketi halali na mchezo kuvunjwa bila kutolewa ufafanuzi wowote wa namna ya kuwafidia?

6. Je,Taasisi iliyotaka kusogeza mbele muda wa mchezo walishirikiana vipi na TFF walifanya juhudi gani za kuwatafuta viongozi wa klabu kisha kuwa na makubaliano?

7. Kama taasisi iliyotaka kusogeza mbele muda wa mchezo ipo ndani ya serikali ilifanya mawasiliano ya njia gani na TFF ambazo itawabeba TFF?

8. TFF ndio iliyotoa taarifa ya kusogeza mbele muda wa mchezo lakini Rais wa TFF amenukuliwa akisema hajui kilichotokea,je tafsiri yake ni nini?

9. TFF ndio walitoa taarifa ya mechi kuahirishwa kwa kile walichodai maelekezo kutoka serikalini. TFF haohao jana wakatoa taarifa ya kusikikitishwa na mechi kutochezwa huku wakiilekeza bodi kutoa taarifa za kina juu ya kilichopelekea mechi kuahirishwa, je walidanganya mashabiki?

10. Ni wao TFF waliotoa taarifa mechi itasogezwa mbele hadi saa 1 usiku. Kwa nini marefa hawakuikagua Simba?

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz