Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa wengine hawa hapa wanamsubiri Amunike awaite

17750 Pic+mastaa TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Timu ya Taifa la Tanzania ‘Taifa Stars’ inaweza kuwa miongoni mwa mataifa 24 yatakayoshiriki mwakani kwenye Fainali za Afcon zitakayofanyika mwakani nchini Cameroon kuanzia Juni 7 hadi 30.

Taifa Stars ambayo ipo Kundi L, baada ya kuibana kwao Uganda na kurejea nchini wiki iliyopita na pointi moja, itakuwa na kabarua kingene kwenye mchakato wa kuwania ticketi ya Afcon, Oktoba 12 dhidi ya Cape Verde.

Timu hiyo ya taifa kwenye mchezo uliopita ilikuwa na wachezaji tisa wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi ambao ni Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji, Saimon Msuva wa Difaa El (Jadida, Morocco), Farid Mussa na Shaaban Chilunda wa Tenerife ya Hispania.

Wengine ni Himid Mao (Petrojet, Misri), Rashid Mandawa (BDF XI, Botswana), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Hassan Kessy (Nkana Red Devils, Zambia) na Thomas Ulimwengu wa Al Hilal ya Sudan.

Spoti Mikiki ambayo siku zote imekuwa mstari wa mbele kuvumbua wachezaji wa Tanzania wanaocheza nje ya nchi, inakuletea nyota wengine wanaocheza mara kwa mara kwenye ligi za mataifa yaliyoendelea.

Nyota hao wanaweza kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Emmanuel Amunike ambaye ameonekana kuwa na imani juu ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi hasa wale ambao wanacheza kwenye ligi kubwa zenye ushindani zaidi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Orgeness Mollel/Tirsense (Ureno)

Winga wa zamani wa FC Famalicao ya daraja la kwanza Ureno, Orgeness Mollel ambaye amejiunga na Tirsense ya daraja la pili nchini humo, anaweza kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Taifa Stars kama ataitwa kwa mara nyingine.

Awamu ya kwanza kwa winga huyo mwenye umri wa miaka 20 kuitwa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ilikuwa chini ya Salum Mayanga lakini hata hivyo hakutua nchini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake.

Mollel amewahi kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ pamoja na beki wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’.

Yahya Al Ghanassi - Al Wahda, Falme za Kiarabu

Yahya Ali Said Al Ghassani ni Mtanzania ambaye hivi karibuni amesaini mkataba wake wa kwanza wa kucheza soka la kulipwa baada ya kufanya vizuri akiwa na kikosi cha timu ya vijana.

Ghassani amesaini mkataba wa miaka mitano ambao utamalizika 2023 akiwa na miamba hiyo ya soka inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo, tayari mshambuliaji huyo ameifungia bao moja timu yake katika michezo miwili aliyoichezea Al Wahda inayonolewa na Lauren?iu Reghecampf mwenye uraia wa Romania.

Adolf Bitegeko-KR Reykjavík (Iceland)

Adolf Bitegeko ni kiungo mkabaji anayecheza soka la kulipwa Iceland kwenye klabu iitwayo KR Reykjavík inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo, nyota huyo alianza kucheza soka lake nchini kwenye akademi ya Azam, Chamazi kisha akapata nafasi Marekani ambako alikuwa akicheza soka la vyuo.

Adam Kasa - Enskede (Sweden)

Mjukuu wa kipa wa zamani wa Simba, Athumani Mambosasa (sasa marehemu), Adam Kasa ni beki wa kushoto anayecheza Ligi Daraja la Tatu, Sweden naye anaweza kutumika kutokana na uzoefu alionao wa kucheza soka la kimataifa.

Hamis Abdallah - Bandari (Kenya)

Miongoni mwa wachezaji kutoka nje ya nchi ambao walikuwa wakipata nafasi chini ya Salum Mayanga alikuwa ni Hamis Abdallah ambaye kwa kipindi hicho alikuwa akiichezea Sony Sugar. Hamis amekuwa kwenye kiwango bora ambacho kimeisaidia Bandari anayoichezea kwa sasa kuwa miongoni mwa timu zinazotisha kwani inashika nafasi ya pili nyuma ya Gor Mahia ambayo tayari imeshatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Kenya.

Ayubu Lyanga - Zanaco (Zambia)

Ayubu Lyanga ni kiungo wa Kitanzania anayeichezea Zanaco ya Ligi Kuu Zambia, kiungo huyo anaweza kuiongezea nguvu Taifa Stars ya Amunike kama ataamua kumwita kwenye kikosi chake.

Juma Byabusha-Binghamton FC (Marekani)

Juma Byabusha ni kiungo anayefananishwa na Bakayoko wa Chelsea aliyejipatia umaarufu mkubwa akiwa na Monaco, Juma anayeichezea Binghamton FC ya daraja la tatu Marekani (NPSL) amekuwa akitajwa kuwa kwenye kiwango bora kwa sasa.

Taarifa tulizonazo ni kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 ameanza kuhusishwa na kujiunga na New York City FC ya Ligi Kuu Marekani mara baada ya kumaliza shahada ya uhandisi katika chuo kikuu cha Binghamton.

Chanzo: mwananchi.co.tz