Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masoud apigwa chini safari ya Simba Mwanza

17855 Pic+masoud TanzaniaWeb

Tue, 18 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Djuma ameachwa tena katika safari ya timu hiyo inayokwenda Mwanza mapema kesho asubuhi kuivaa Mbao na Mwadui.

Katika orodha ya wachezaji 21, wataondoka katika safari hiyo akiongezeka mmoja kati ya wale 20, walikwenda Mtwara.

Msafara wa Simba aliokwenda Mtwara kucheza dhidi ya Ndanda Djuma hakuwa miongoni mwa mwao na alipewa maagizo na kocha mkuu Patrick Aussems kubaki na wachezaji wa timu za vijana.

Djuma hatakuwa tena sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kitakwenda Mwanza kesho Jumanne kwa ajili ya mechi dhidi ya Mbao na Mwadui huko kanda ya ziwa.

Djuma alisema atabaki na wachezaji wasiokwenda huko Mwanza na wanatakiwa kufanya mazoezi kama ilivyo kawaida.

"Sina taarifa za kwenda ila nafahamu nitabaki hapa Dar es Salaam na sitakwenda kanda ya ziwa kwani natakiwa kusimamia mazoezi ya wachezaji ambao nitabaki nao," alisema Djuma.

Chanzo: mwananchi.co.tz