Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masoud Djuma kuiongoza Simba Taifa leo

20078 Pic+djuma TanzaniaWeb

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam:  Yule kocha kipenzi cha mashabiki wa Simba, Mrundi Masoud Djuma, baada ya kuwekwa pembeni katika michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara kwa mara nyingine, leo Jumapili watakapokuwa wanapambana na Yanga atakuwepo benchi.

Djuma ambaye ilidaiwa hana maelewalo mazuri na Aussems ndiyo sababu iliyomfanya abaki Dar es Salaam wakati kikosi hicho kimekwenda kucheza mechi za nje mikoani.

Hakuwa na timu ilipochezwa Mtwara na Ndanda FC wakamaliza kwa suluhu, alikosa mechi ya Ndanda FC ambayo walifungwa bao 1-0 na ule wa Mwadui FC walioibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Hii ni baada ya kupewa program maalum ya kusimamia wachezaji waliobaki Dar es Salaam pamoja na kuisoma Yanga katika mechi zao.

Chanzo: mwananchi.co.tz