Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masikini Wawa ndiyo basi tena kuikosa TP Mazembe nje wiki mbili

51327 Pic+wawa

Wed, 10 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Beki wa kati wa Simba, Pascal Wawa ataikosa mechi ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya TP Mazembe baada ya kutakiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili.

Wawa aliumia katika dakika 5, katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam na kutolewa nje nafasi yake kuchukuliwa na Jjuuko Murshid katika mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu.

Akizungumzia afya yake Wawa alisema amefanya vipomo na ameambia anatakiwa kuwa nje ya uwanja wa wiki zisizopungua mbili.

Alisema nitakuwa nje ya uwanja wa wiki mbili ambazo natakiwa kupumzika bila kufanya mazoezi yoyote.

"Nimefanya vipimo ni nyama za paja zimeachia ambazo nimeshaanza tiba yake, lakini Daktari ameaniambia nikae nje ya Uwanja wiki mbili nipumzike sana bila kufanya mazoezi," alisema Wawa.

"Baada ya hapo nitarudi tena hospitali ili kuangalia vipimo vingine kama nitaweza kuanza mazoezi mapesi mepesi au nibaki tena nje," alisema.

"Kwangu nashukuru naendelea vizuri tofauti na siku ya kwanza maumivu yamepungua ndio maana nimefika mpaka kuona mazoezi ya wenzangu," alisema.

"Sitakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitakwenda DR Congo kwani bado nitakuwa nje ya uwanja ingawa malengo yangu nilikuwa naitamani sana mechi hiyo kutoa mchango kwa timu yangu kupata kile ambacho tumekipanga.

"Mwisho niwatakie kila la kheri wenzangu katika mechi na Mazembe lakini pia nashukuru maendeleo yangu yanazidi kuwa mazuri kila siku," alisema Wawa.

Wawa alikosekana katika katika mazoezi ya Simba ambayo yalifanyika asubuhi ya leo katika uwanja wa Gymkhana.

Wawa mbali ya kushindwa kufanya mazoezi hayo, lakini alijitokeza uwanjani hapo akiwa na amevaa nguo za nyumbani ma miwani akifatilia wenzake wakifanya mazoezi.

Mara baada ya mazoezi kumalizika Wawa aliongea na kocha Patrick Aussems kisha akapanda kwenye gari yake akaondoka.



Chanzo: mwananchi.co.tz