Mashindano ya London Marathon ambayo ilisimama kutokana na janga la corona sasa inarudi rasmi mitaani kesho tarehe 3 Oktoba.
Africa inawakilishwa vyema na wanariadha maarufu akiwemo mkenya Brigid Kosgei na Muethiopia Shura Kitata ambao wote watakuwemo kwenye mstari wa kuanzia.
Takribani wakimbiaji 40,000 watajiunga na wanariadha maarufu kukimbia kuanzia Blackheath na kumalizia maili 26.2 baadae katika eneo la Buckingham Palace.
Mkurugenzi mkuu wa London Marathon Hugh Brasher amesema mbio hizo kwa mwaka huu zinaweza kuwa zenye kuleta kumbukumbu kubwa kuliko zote kuwahi kutokea,ambapo ni takribani miaka 40 tangu kuanza kwa mbio hizo rasmi mwaka 1981.
"Hii sio tu Marathon bali ni kuwaleta watu pamoja, kitu ambacho tulikimiss saana".