Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wazidi kuzimia Lake Tanganyika

Zimia Pic Data Mashabiki wazidi kuzimia Lake Tanganyika

Mon, 26 Jul 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MASHABIKI sita wakiwa ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika wamepoteza fahamu na kubebwa katika machela na watu wa huduma ya kwanza.

Mashabiki hao walizimia kwa nyakati tofauti kutokana na sababu ambazo hazikujulikana kwa haraka.

Watu hao walionekana kuwa wanne wamevalia jezi za Yanga na wawili walikuwa wamevaa Jezi ya Simba.

Wale wa Yanga, wakiwa wamebebwa katika machela na watu wa huduma ya kwanza, wakipita katika eneo ambalo mashabiki wa Simba wamekaa walikuwa wakiwazomea.

Hivyo hivyo kwa shabiki mmoja wa Simba alipobebwa na watu wa huduma ya kwanza mashabiki wa Yanga nao walimzomea vile vile.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz