Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wasubiria staili ya ushangiliaji wa Makambo

Makambo Pic Data Mashabiki wasubiria staili ya ushangiliaji wa Makambo

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MASHABIKI wa Yanga, wana raha na ujio wa straika wa kimataifa, Heritier Makambo wakitarajia atarejesha kicheko cha staili yake ya ushangiliaji.

Makambo msimu wa 2017/2018 aliofunga mabao 17 alikuwa anashangilia kwa staili ya kutimia mikono miwili kama anajaza kitu, wakati Meddie Kagere wa Simba alikuwa anafumba jicho moja.

 Anwari Mwita 'Yanga Kigelegele' ni shabiki kindakindaki wa Yanga, amesema msimu ujao utakuwa wa kusikika makofi uwanjani, Makambo akiwa amefunga.

Amesema staili yake ya ushangiliaji ilikuwa inawapa raha mtaani ya kuwakera watani wao wa jadi Simba.

"Msimu ujao nauona utakuwa wa kicheko na raha, kutokana na ufundi wa Makambo kutupia nyavu na kubuni staili nzuri ya kushangilia iliyokuwa inatupa raha mashabiki wake, karibu sana Makambo"amesema Yanga Kigelegele.

Kauli yake imeungwa mkono na msanii wa bongo fleva, Z Anto amsema kwa namna anavyoipenda Yanga, amefurahisha na ujio wa Makambo fundi wa mabao.

"Ukisikia ujazo wa mabao na makofi unajua Makambo kasababisha aje tu, ili tupate cha kutamba nacho mtaani mbele ya watani wetu wa jadi,"amesema

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz