Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wakauka uwanjani, Simba yagawa dozi

10443 Kagam+pic TanzaniaWeb

Sun, 1 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea Russia yamefanya Kombe la Kagame kupoteza mvuto kwa mashabiki kujitokeza viwanjani kushudia mechi kwenye Uwanja wa Azam Complex na Uhuru Dar es Salaam.

Katika mechi za jana za ufunguzi zilishudiwa na mashabiki wachache hali hiyo ilitegemewa kuwa tofauti leo wakati mabingwa wa Ligi Kuu, Simba ikiwa na wachezaji wapya dhidi ya  Dakadaha, lakini mashabiki waliofika uwanjani ni wachache.

Simba inaongoza kwa mabao 4-0 yaliyofungwa na Marcel Kaheza dakika ya tisa na Adam Salamba dakika ya 15, 76 na Rashid Juma dakika ya 45.

Pamoja na ushindi huo shamla shamla za mashabiki sio kubwa, tofauti na ilivyozoeleka.

Kitu kikubwa kwa mashabiki ni mjadala wa wachezaji wao wapya kama Pascal Wawa kuona anafanya maajabu.

Huku wakiwa na hamu kuona mshambuliaji Meddie Kagere anakuwa na jipya na kuonyesha uzoefu kuliko kiwango cha Salamba, Kaheza na Juma kwa kuzitumia vema nafasi wanazopata.

Hata hivyo mashabiki hao wanaonekana kumwamini zaidi Wawa kwa kuona atakuwa nguzo ya safu ya ulinzi ndani ya kikosi hicho

Chanzo: mwananchi.co.tz